Picha mpya za satelaiti za kambi ya wakimbizi ya Shimelba iliyoko kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia zinaonyesha zaidi ya miundombinu 400 imeaharibiwa vibaya katika kile ambacho makundi ya watafiti yanaamini kwamba ni mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na wanamgambo wa nje ya Ethiopia na huenda wakawa ni kutoka Eritrea.
Ripoti iliyotolewa na shirika la DX Open Network yenye makao yake nchini Uingereza iliyosambazwa na shirika la habari la AP inasema inawezekana kwamba tukio la moto la Januari 16 ni moja ya mlolongo wa matukio ya uvamizi wa kijeshi dhidi ya kambi hiyo kama ilivyoripotiwa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Marekani.
Ripoti hiyo mpya imesema kuna uwezekano kwamba washambuliaji waliganyika kwa makundi na kwenda mlango ka mlango kuwasha moto kwenye majengo, sawa sawa na mashambulizi ya siku za nyuma yaliyofanyika kwenye kambi ya Hitsats ambayo pia haifikiki kwa urahisi.