Polisi Uganda yathibitisha kumuweka kizuizi cha nyumbani Bobi Wine




Wasemaji wa jeshi na polisi nchini Uganda wamesema mpinzani wa rais Yoweri Museveni Robert Kyagulanyi Bobi Wine ataendelea kukaa katika kizuizi cha nyumbani kwa muda usiojuliakana. 
Vyombo hivyo vya usalama vimedai kuwa na taarifa kuwa akiwa huru, Bobi Wine anapanga kuwachochea vijana kishiriki katika ghasia. 

Polisi pia imethibitisha vifo vya watu wanne ikiwemo mama mjamzito kufuatia makabiliano yaliyozuka mjini Masaka kati ya wafuasi wa mwanasiasa huyo na wanajeshi. 

Bobi Wine na chama chake cha NUP wanayapinga matokeo ya uchaguzi uliomrejesha madarakani rais Yoweri Museveni na kuahidi kuyapinga mahakamani. 

Wagombea wengine wa urais nao wamepinga matokeo hayo wakisema idadi ya wapiga kura ilikuwa kubwa tofauti na takriban watu milioni 10 waliotajwa kushiriki. 

Kulingana na tume ya uchaguzi waliosajiliwa kupiga kura ni watu zaidi ya milioni 18.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad