Pompeo na familia yake wapigwa marufuku kuingia China




China imewawekea vikwazo Maafisa 28 waliokuwa kwenye utawala wa Rais Trump akiwemo Waziri wa Mambo ya nje aliemaliza muda wake, Mike Pompeo, taarifa toka Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema maafisa hao walikiuka haki ya China kama taifa huru.
Hatua hii inakuja ikiwa ni baada ya Mike Pompeo kupitia ukurasa wake wa Twitter kunukuliwa akisema “Chama cha Kikomunisti cha China sio rafiki yetu” kauli ambayo inatajwa kuikera China.

Vikwazo hivyo vinawazuia maafisa hao na familia zao kuingia China, Hong Kong na Macau huku taasisi yoyote yenye uhusiano nao kutoruhusiwa kufanya biashara China.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad