Prof Jay "Mimi ni Mbunge nje ya Bunge"



JOSEPH Haule, maarufu Profesa Jay amesema, yeye ni mbunge nje ya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema hayo leo Alhamisi tarehe 14 Januari 2021, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM alipokwenda na Stamina kutambulisha wimbo wao mpya unaoitwa ‘Baba.’


Profesa Jay alikuwa Mbunge wa Mikumi Mkoa wa Morogoro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kati ya mwaka 2015-2020 ambapo katika uchaguzi mkuu uliopita, alishindwa kutetea nafasi yake.

Akijibu swali aliloulizwa kwa sasa yeye si mbunge, nini kinaendelea, amesema “ubunge si lazima kuwa bungeni, mbunge ni kuwawakilisha wananchi. Kwa kuwa nimewahi kuwa mbunge wa Mikumi kwa hiyo, unaweza kuendelea kuniita mbunge nje ya Bunge. Mimi ni mgodi unaotembea.”


Bobi Wine
Profesa Jay ambaye ni msanii wa Hip Hop amesema, anaendelea na harakati ndani ya jimbo hilo akisisitiza hata Studio ya Wanalizombe aliyoijenga Mikumi “itaendelea kuwa Mikumi” ili kuinua vipaji mbalimbali jimboni humo.


Alipoulizwa kuhusu mgombea urais wa Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bob Wine kama anamuunga mkono, Profesa Jay amesema, “mimi nimekuwa rafiki na Bob Wine kitambo sana.”

“Tunafurahi kusikia vijana wanakwenda kwenye ngazi za maamuzi. Sisi tunamuunga mkono Bob Wine na Jose Chamilioni anagombea huko. Vijana wanapokwenda kwenye vyombo vya uamuzi ni jambo zuri,” amesema Profesa Jay


Wananchi wa Uganda, leo Alhamisi wanapiga kura katika uchaguzi mkuu nchini humo.



Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zari la Mentali, Umetisha Aisee, Ningekuomba kama tutaweza kumshirikisha
    Kolabo moja Chagulanyi,tumsaidie kupanua kipaji chake hata studio ya Mikumi
    itakua poa, pia atapata kufanya Utalii mbugani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad