Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga Mganga Mkuu wa Serikali apatiwe cheti cha COVID 19

 


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma inamshikilia bwana Alexander Mwikali (42) mkazi wa Nkuhungu Dodoma kwa kosa la kujaribu kutoa hongo ya shilingi laki mbili (200,000) kwa Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi ili apatiwe cheti cha kuthibitisha kuwa hana Virus vya COVID 19.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dodoma kutoa taarifa ya utekelezaji kwa robo  ya mwaka Octoba hadi Disemba 2020, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema walimkamata bwana Alexander Mwikali ambaye ni mtaalamu wa nyama wa Kampuni ya Alkafil.


Akijaribu kutoa rushwa kwa mganga mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi kama kishawishi ili ampatie cheti cha uthibitisho wa kutokuwa na ugonjwa wa virus vya Corona.


" Mtuhumiwa alitaka cheti hicho ili aweze kusafiri nje ya nchi na tayari tumemfikisha katika mahakama ya mkoa wa Dodoma na kulipa faini ya laki tano(500,000)" amesema Kibwengo.


Pia TAKUKURU Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 13 wa mwaka wa tatu 3 wa  chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini cha Jijini Dodoma kwa kujihusisha na udanganyifu wakati wa kufanya mitihani ya marudio.


Amesema katika uchunguzi wao umeonyesha wanafunzi hao kwa kutumia rushwa waliweza kufanya mitihani hiyo nje baada ya kumaliza mitihani halali na kujaribu kubadilisha katika mitihani ya awali.


"Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba wanafunzi hao kutumia rushwa waliweza kurudia mtihani huo nje ya chumba cha mtihani na kujaribu kuingiza karatasi hizo katika mfumo rasmi na kukamatwa na chuo" amesema.


Aidha TAKUKURU imewataka bwana Evalist Nyaki na Lameck Kawinga ambao walikuwa wanafunzi wa Chuo hicho kuripoti katika ofisi za TAKUKURU kusaidia uchunguzi wa tukio hilo wakituhumiwa kuhusika.


Pia TAKUKURU Mkoa wa Dodoma inaendelea na uchunguzi dhidi ya Kampuni ya ukopeshaji ya Geneva Credit shop ya mjini Kondoa kwa kutoa mikopo umiza na TAKUKURU imepokea malalamiko ya wananchi 30 kwa madai ya kupatiwa mikopo umiza.


Amesema katika uchunguzi uliofanya na TAKUKURU umeonyesha pamoja na kufanya biashara kwa miaka 25 lakini ilisajiliwa rasmi Octoba, 2016 na kwamba haikuwa inalipa kodi ya Serikali na wengi waliokopeshwa ni watumishi wanaokaribia kustaafu.


Ameongeza kuwa "Kamati ya usalama Wilaya ya Kondoa katika kufuatilia swala hilo imekamata kadi za benki (ATM Card) zaidi ya 400 zikiwa zimeshikiliwa na mmiliki wa kampuni hiyo bwana  Abubakary Kinyuma maarufu kama Abubakary Mapesa ambaye mpaka sasa anatafutwa na taasisi hiyo.


Katika kufuatilia fedha za Umma na miradi ya Maendeleo wamewezesha kuokoa au kudhibiti shilingi 283.9 pamoja na viwanja 14 na shamba moja miongoni mwa fedha hizo ni mikopo umiza, madeni ya vyama vya akiba na mikopo na mishahara hewa.


Pia wamefanikiwa kugundua shilingi milioni mia tano (500,000) hazikulipwa na makampuni ya ujenzi wa miondombinu ya maji na barabara hayakulipa kodi na kuzisababishia hasara halmashauri ya shilingi milioni mia tano (500,000).


Aidha TAKUKURU imewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa zinazohusu vitendo vya rushwa na kuualifu Umma wa wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuwa wameanza program ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu rushwa kwa kila siku za jumanne ya kwanza ya mwezi na jumanne ya mwezi wa pili watakuwa na TANESCO kusikiliza na kutatua kero zinazohusu uunganishwaji wa huduma za umeme.


 



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad