Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza shamba la miti Chato mkoani Geita kupewa jina la Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo kutokana na utendaji wake uliowezesha kulifufua shamba hilo na kuacha kutumia jina la Shamba la miti la Chato.
Shamba la miti la Chato lenye ukubwa wa hekta 69,000, lilianzishwa mwaka 2017 baada ya uharibifu mkubwa uliofanywa na wanachi kuvamia shamba hilo na ndipo serikali kupitia wakala wa misitu (TFS), wakaamua kuendeleza shamba hilo ili kutunza mazingira.
“Shamba hili badala ya kuitwa shamba la miti Chato litaitwa shamba la miti Silayo ili wajukuu wako na watu wengine wakumbuke mtu ukifanya kazi nzuri utakumbukwa, Silayo umeweka alama na hili shamba la Hekari 69, 000 linastahili kuitwa jina lako”- Rais Dk John Magufuli
“Ifike mahali watu wanapofanya kazi nzuri wakumbukwe kwa kazi zao tunapenda mashamba na vitu mbalimbali kuitwa majina ya wanasiasa kwahiyo Profesa Dos Santos Silayo nafikiri mamlaka hayo ninayo kwamba shamba hili baada ya kuitwa Shamba la Miti Chato sasa litaitwa Shamba la Miti Silayo.”– Rais Dk John Magufuli.