Afisi ya rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema Rais Felix Tshisekedi amewapa msahama wa rais watu ishirini na sita waliokuwa wamefungwa jela kwa njama ya kumuua rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Kabila.
Watu hao walihukumiwa kifo na maafisa wanasema baadhi wamefariki wakiwa gerezani ila hakuna hata mmoja ambaye amenyongwa. Laurent Kabila aliuwawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake katika kasri lake mwezi Januari mwaka 2001.
Mara tu baada ya kumuua, mlinzi huyo naye aliuwawa kwa kupigwa risasi. Mtoto wa Laurent, Joseph Kabila mara kadhaa alikataa wito wa kuwasamehe watu hao waliofungwa kwa kumuua babake.
OPEN IN BROWSER