Rais Recep Tayyip ErdoÄŸan alifanya mawasiliano kwa njia ya simu na Furkan Yaren ambaye ni mmoja wa manahodha wa meli iliyoshambuliwa na maharamia wa Nigeria.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Rais, ErdoÄŸan, ambaye alifuatilia kwa karibu maendeleo yote juu ya suala hilo, alipokea taarifa juu ya hali ya afya ya wafanyikazi 3 ambao walinusurika kwenye shambulizi la meli iliyotia nanga Gabon na kuwasilisha ujumbe wa kuwatakia afueni ya haraka.
Rais ErdoÄŸan alisema kuwa mipango ya uokoaji inaendelea kwa juhudi zote ili kuwarejesha wafanyikazi waliotekwa nyara.
Kwa upande mwingine, Balozi wa Uturuki mjini Libreville Nilüfer Erdem Kaygısız, pia aliwasiliana na wafanyikazi 3 wa meli ya "Mozart" ya Kituruki, iliyokuwa imetekwa nyara na maharamia.
Meli yenye bendera ya Liberia iitwayo Mozart ilishambuliwa na maharamia hapo jana karibia maili 180 kutoka pwani ya Lagos, nchini Nigeria.
Mmoja kati ya wafanyakazi 19 wa meli hiyo iliyokuwa ikitoka Lagos nchini Nigeria kwenda Cape Town nchini Afrika Kusini, aliuawa na watu wengine 15 wakatekwa nyara
Manusura 3 walitia nanga na meli hapo jana katika Bandari ya Gentil nchini Gabon.