Sekondari Baobab yaendelea kung’ara kitaalum



SHULE ya Sekondari Baobab ya Mapinga Bagamoyo imefanikiwa kufaulisha wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne na cha pili .

Akizungumza na Michuzi Blog shuleni hapo, Mkuu wa shule hiyo, Venance Hongoa amesema matokeo hayo ni mazuri sana kwao kwasababu wamekuwa wakichukua wanafunzi wenye ufaulu wa kawaida sana na kuwawekea mikakati madhubuti ili kuinua ufaulu wao.

Amesema kwenye matokeo ya kidato cha nne wanafunzi 113 wamefaulu kwa daraja la kwanza, wanafunzi 74 daraja la pili, wanafunzi 26 daraja la tatu na watatu tu ndio wamepata daraja la nne huku kwenye matokeo ya kidato cha pili wanafunzi 221 wamepata daraja la kwanza, wanafunzi 46 wamepata daraja la pili na wanafunzi 10 wamepata daraja la tatu.

Amesema wengi wa wanafunzi wanaowachukua ni wale waliofanya usaili shule nyingine na wakakosa nafasi.

“Sisi tunachukua wanafunzi wa kawaida sana na kuwaandaa na sasa wamefaulu vizuri sana; tunajivunia kwa hilo kwani kuna wenzetu huchukua wanafunzi wenye vipaji sisi huwa hatuangalii hilo...., wanafunzi wengi wanaoingia shuleni hapa wanaingia na wastani wa “C” lakini wamemaliza kwa kupata alama za juu za “A” na “B” katika masomo mbalimbali kwenye matokeo ya mwaka huu na wazazi wamefurahi sana", amesema

“Kwa kulinganisha na walivyoingia na matokeo haya ni mafanikio makubwa sana kwetu na kazi kubwa sana imefanyika tunashukuru juhudi za walimu na ushirikiano wa wazazi, uongozi wa shule na wanafunzi wenyewe, uongozi nao umeweka mazingira wezeshi ya kujifunza na kufundisha” alisema

Ameongeza kuwa, hata kwenye matokeo ya kidato cha sita  wamekuwa wakifaulisha wanafunzi wengi kwa daraja la kwanza na la pili kutokana na jitihada kubwa inayofanywa na walimu na uongozi wa shule hiyo.

“Tunashukuru kipekee uongozi wa shule na walimu kwa namna wanavyotupa ushirikiano mkubwa kuhakikisha shule yetu inaendelea kuwa juu mwaka hadi mwaka tunawaomba waendelee kutupa ushirikiano kama huo ili Baobab izidi kuwa juu,” alisema

Aidha ametaja siri ya mafanikio hayo kuwa ni mazingira bora ya kufundishia yaliyowekwa na uongozi wa shule hiyo kwa walimu na wanafunzi ikiwemo maabara na maktaba za kisasa za shule hiyo.

“Huduma bora za chakula, malazi,  na zahanati iliyoko ndani ya shule ni miongoni mwa vichocheo vya mafanikio yetu tumehakikisha afya imara za wanafunzi maana hawahitaji kwenda nje ya shule kwa matibabu wanatibiwa hapahapa.".


Wanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Baobab ya Mapinga Bagamoyo wakisikiliza mawaidha kutoka kwa mwalimu wao Samwel Sanga baada ya wanafunzi  221 wa shule hiyo kufaulu kwa daraja la kwanza na 46 daraja la pili kwenye matokeo ya kidato cha pili yaliyotangazwa hivi karibuni na wenzao 113 wa kidato cha nne kupata daraja la kwanza.

Wanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Baobab ya Mapinga Bagamoyo wakifurahia baada ya kutangaziwa matokeo yao kuwa mazuri na wanafunzi 221 wa shule hiyo kufaulu kwa daraja la kwanza na 46 daraja la pili kwenye matokeo ya kidato cha pili yaliyotangazwa hivi karibuni na wenzao 113 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad