Serikali Yapiga Marufuku Kuchukua Ardhi Bila Kulipa Fidia

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amepiga marufuku halmashauri, Taasisi na Watu binafsi kuchukua maeneo ya wananchi bila kulipa fidia.

Akizungumza hivi karibuni mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa huo, Lukuvi alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya halmashauri na Taasisi kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa fidia kwa maelezo maeneo hayo kuhitajika kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo.

Kwa mujibu wa Lukuvi, sheria inakataza kuchukua maeneo ya wananchi bila kulipa fidia na Mhe. Rais John Pombe Magufuli alishakataza watu, taasisi au halmashsuri kunyang’anya maeneo ya wananchi bila kulipa fidia.

Waziri Lukuvi alifikia kutoa maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Bibi Maria Samweli mkazi wa Singida ambaye alimpa malalamiko yake ya kutolipwa fidia kwa zaidi ya miaka 12 kwa ajili ya kupisha mradi wa upimaji na ugawaji viwanja.

” Mtu yeyote atakayeendeleza maumivu kwa wananchi kwa kuendeleza kero ya kuchukua maeneo bila kulipa fidia kazi yake itakuwa kubwa, kwanza msisitizo ulishawekwa na Mhe Rais Magufuli aliyepiga marufuku watu, taasisi au halmashauri kupora maeneo ya wananchi bila kulipa fidia” alisema Lukuvi.

Alisema, upo utaratibu wa kuchukua maeneo ya wananchi kwa manufaa ya umma na utaratibu huo lazima mwananchi alipwe fidia kwa kupewa haki yake na kusisitiza kuwa ardhi pekee inayoweza kuchukuliwa bila kulipa fidia ni ile aliyomilikishwa mtu kwa hati na mmiliki huyo akashindwa kuendeleza kwa wakati ambapo hati hiyo ikifutwa mmiliki wake hawezi kulipwa fidia.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kuwa, halmashauri yoyote ikitamani ardhi inayomilikiwa kihalali na hata kama halijaendelezwa lazima mmiliki wake alipwe fidia na kusisitiza kwamba, tangu mwaka 1999 ardhi isiyofanyiwa kitu chochote ina thamani yake na kilichoendelezwa juu yake nacho kina thamani yake.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lukuvi, Umenena tunayotaka kuyasikia. Siyo Dhuuluma za Kiholela.
    Kipenzi chetu JPM anajua maumivu yetu na hali zetu.

    Wengine sasa hivi tumesha staafu uwezo umekuwa mdogo, watoto zetu hawana ajira za maana. Tunahangaika nenda rudi za mafao yetu badoo.

    Ndio ukaona Mh Kassim Majaliwa alipokuwa Kigoma cha kwanza yule mama aliambiwa pimeni eneo mnalolitaka mumpe haki yake haalaafu mkamilishe mradi. Hii ndio Haki na Uadilifu tunao utaka Watanzania.

    Katika kufuata nyayo za Magufuli, Raisi waa Marekani baada ya uteuzia wa safu yake ya Uongozi, Aliwakumbusha wateuliwa wake na kusisitiza kwamba.

    Watu/Wananchi haawatufanyii kazi Sisi nikiwemo mimi(Joe Biden) ni Sisi tunawafanyia kazi Watu(Wananchi) na asiyeweza kuzungumza nao kwa Heshima na Ukarimu sito sita kumwachisha papo hapo (Kumtumbua).

    Nakumbuka, JPM alivyo fika Kwenye Daraja na kutolea ufumbuzi yeye mwenyewe
    baada ya watu kukaa barabarani masiku, Cha kwanza alichofanya alituomba Radhi sisi Wananchi kwa Usumbufu uliotokea na ufumbuzi kusua sua kwa Masiku. Hizi ndio leadership Qualities second to Non. Lukuvi Asante sana.

    Magufuli Baba, Allah akulinde na kukujaza Kheri na Baraka.

    ReplyDelete
  2. Lukuvi, Umenena tunayotaka kuyasikia. Siyo Dhuluma za Kiholela.
    Kipenzi chetu JPM anajua maumivu yetu na hali zetu.

    Wengine sasa hivi tumesha Staafu uwezo umekuwa mdogo, watoto zetu hawana ajira za maana. Tunahangaika nenda rudi za mafao yetu badoo.

    Ndio ukaona Mh Kassim Majaliwa alipokuwa Kigoma cha kwanza yule mama aliambiwa pimeni eneo mnalolitaka mumpe haki yake haalaafu mkamilishe mradi. Hii ndio Haki na Uadilifu tunao utaka Watanzania.

    Katika kufuata nyayo za Magufuli, Raisi waa Marekani baada ya uteuzia wa safu yake ya Uongozi, Aliwakumbusha wateuliwa wake na kusisitiza kwamba.

    Watu/Wananchi haawatufanyii kazi Sisi nikiwemo mimi(Joe Biden) ni Sisi tunawafanyia kazi Watu(Wananchi) na asiyeweza kuzungumza nao kwa Heshima na Ukarimu sito sita kumwachisha papo hapo (Kumtumbua).

    Nakumbuka, JPM alivyo fika Kwenye Daraja na kutolea ufumbuzi yeye mwenyewe
    baada ya watu kukaa barabarani masiku, Cha kwanza alichofanya alituomba Radhi sisi Wananchi kwa Usumbufu uliotokea na ufumbuzi kusua sua kwa Masiku. Hizi ndio leadership Qualities second to Non. Lukuvi Asante sana.

    Magufuli Baba, Allah akulinde na kukujaza Kheri na Baraka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad