Waziri wa Kilimo. Prof. Adolf Mkenda amesema, Uzalishaji wa Sukari umeongezeka kutoka tani 295,775 mwaka 2015/2016 hadi tani 377,527 zinazotarajiwa kuzalishwa Msimu wa 2020/2021.
Katika Msimu wa 2020/2021, tani 377,527 za Sukari zinatarajiwa kuzalishwa kwenye Viwanda vilivyopo Nchini vikiwemo Kilombero Sugar Company Ltd, Mtibwa Sugar Estate, Kagera Sugar Ltd, TPC Ltd na Manyara Sugar Ltd.
Waziri huyo amesema, mahitaji ya Sukari kwa matumizi ya kawaida na Viwandani ni tani 655,000 kwa mwaka, hivyo ili kuongeza uzalishaji Serikali imepanga kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa Wakulima wadogo.
Ameongeza kuwa, kutokana na mafanikio hayo katika ongezeko la uzalishaji, Tanzania bado ina uhitaji wa kuagiza Sukari kutoka nje ya Nchi kiasi cha Tani 40 kwa kuwa bado Viwanda vya Ndani havijitoshelezi katika uzalishaji wake.