Serikali yatoa Neno Kuhusu zuio la Watanzania Kuingia Uingereza

 


Mkurugenzi wa Habari Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, amesema kuwa wao hawana taarifa rasmi kwamba Uingereza imepiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo na kueleza kuwa hayo ni mambo ya mitandaoni na wao hawayafuatilii.



Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, na kulia ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps


Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 23, 2021, wakati akizungumza na EATV&East Africa Radio, na kuongeza kuwa serikali inao utaratibu maalum wa kupokea taarifa hizo za namna hiyo na kwamba ingekuwa vyema zaidi kama Ubalozi wa Uingereza ungeulizwa kama hiyo kauli ni ya kwao. 


"Utaratibu wa serikali ni kwamba kuna utaratibu wa kuwasiliana, kwahiyo hayo mambo ya kwenye mitandao hatuwezi kuyazungumzia, mimi binafsi nimeiona kama wewe ulivyoiona, serikali haiwasiliani kwenye mitandao bali ina utaratibu wake", amesema Buhohela


Aidha Buhohela ameongeza kuwa, "Kwenye mitandao mambo mangapi ya uongo yanayoandikwa, kama tukipata maandishi au document kutoka Uingereza tutalizungumzia, au mngewapigia Ubalozi wa Uingereza kuwauliza kama hiyo kauli ni ya kwao"

Usikubali Kupitwa na Udaku wa Mjini INSTALL App ya UDAKU Special >HAPA ili Tuwe Tunakutumia Moja Kwa Moja Kwenye Simu Yako

Katibu Mkuu wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps, kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika kwamba zuio la wasafiri kutoka Tanzania na DR Congo, limeanza jana Ijumaa Januari 22, 2021, ikiwa ni hatua za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19, kufuatia kuibuka kwa kirusi kipya cha ugonjwa huo nchini Afrika Kusini


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad