Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutaka wizara ya afya kutokukimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO imeitaka nchi hiyo kujiandaa na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, mkuu wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na kanda ya Afrika Mashariki kwa ujumla.
''Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla. Sehemu ya mawasiliano yetu na Tanzania ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa'' anasema Dkt. Moeti.
WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona. Shirika hilo pia limesisita Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya.
Naye katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus anasema anaunga mkono alichosema @MoetiTshidi, anatoa rai hatua dhabiti za kiafya kukabiliana dhidi ya corona zinapaswa kufuatwa na kujiandaa kupokea chanjo.
Nafasi za Ajira , Jiunge na Group Hili la TELEGRAM Usaidiwe Kutafuta Ajira Bonyeza HAPA Kujiunga
Takwimu ni suala la muhimu pia kwa Tanzania kuzitoa, tena baada ya kesi za miongoni mwa wasafiri na wageni katika miezi ya hivi karibuni.
Chanzo: BBC SWAHILI