Sikiliza Kisa Kizito cha Darassa, Ukimya Mpaka Alivyoibuka Upya




RAPA maarufu Bongo, Darassa amesema watu wengi walikuwa wakim-diss kwamba yupo kimya kwa sababu zao binafsi lakini ukweli ni kwamba alikuwa chimbo akiandaa Bonge la Albamu ambayo kwa sasa inatikisa Bongo nzima.

 

Darassa amesema hayo leo Alhamisi, Janauari 7, 2020, wakati akifanya mahojiano na Kipindi cha Bongo 255 cha +255 cha Global Radio wakati akitambulisha albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘A SLAVE BECOME A KING’.

 

 

“Nimeamua kuiita albamu yangu ‘Slave Becomes a King’ kwa sababu tunataka kuleta mabadiliko flani ya kifikra kwenye jamii, hatuwezi kuwa ng’ombe wa maskini siku zote, lazima tufanye vitu ambavyo ipo siku tutaheshimika.

 

 

KATIKA kipindi cha Bongo 255 leo januari 07, tupo na mwanamuziki, Darassa CMG, ambaye ametoa kuachia album yake hivi karibuni aliyoipa

 

 

“Mimi huwa sipendi kufanya vitu vyepesi, napenda kufanya vitu ambavyo vitakuwa vya tofauti, ndivyo nilivyozoea. Studio yoyote ninayoenda kufanya nayo kazi lazima utakuta mafaili yangu ya muziki.

 

 

 

“Sitaki kuona washkaji zangu wanakaba, wanaiba mtaani, sitaki kuona watu wanakuwa wanyonge ama wanalia, lazima tu-fight, haya ni maisha sio kila siku tunaimba ngoma za huzuni, sipendi kutia huruma, lazima tufurahie pia,” amesema Darassa.

 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad