Hatma ya wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Simba SC kujulikana hii leo, kwa kujua watakutana na timu zipi kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo, ambapo droo ya upangaji makundi itafanyika hii leo mjini Cairo nchini Misri.
Simba walikata tiketi ya kucheza hatua ya makundi baada ya kuiondoa Plateua United ya Nigeria kwenye mchezo wa hatua ya awali kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0, kwenye hatua iliyopita ambayo ni raoundi ya kwanza wakaitupa nje ya mashindano FC Platnum ya Zimbabwe kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 kwenye michezo ya mikondo miwili.
Kikosi hicho cha wekundu wa msimbazi pia kimeweka rekodi ya kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili ndani ya misimu 3, kwani msimu wa 2018-19 walifuzu hatua hii na wakasonga mpaka hatua ya robo fainali lakini wakatolewa na TP Mazembe kwenye hatua hiyo, lakini msimu uliopita waliondoshwa kwenye hatua ya awali na timu ya UD Songo ya Msumbiji.
Droo ya upangaji wa makundi ya michuano hii mikubwa kwa vilabu barani Afrika itafanyika hii leo makao makuu ya shirikisho la soka barani Africa CAF, mjini Cairo nchini Misri majira ya saa 9 alasiri.
Jumla ya timu 16 ndizo zitakazo husika kwenye droo ya upangaji makundi, timu hizo zitapangwa kwenye makundi 4 na kila kundi litakuwa na timu 4.
Timu hizo zimepangwa kwenye vyungu 4 (POT) kulingaana na ubora wa kila timu na kila chungu kina timu 4 na mara baada ya Droo hiyo, michezo yake inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 12 mwaka huu.
Kila chungu kitatoa timu moja moja kwenye makundi yote 4, na mgawanyo wa vyungu hivyo ni kama ifuatavyo
Chungu 1
Al Ahly SC
TP Mazembe
ES Tunis
Wydad Casablanca
Chungu 2
Mamelodi Sundowns
Al Hilal Horoya AC
Zamalek SC
Chungu 3
Al-Merreikh Simba SC
AS Vita Club
Petro Atletico
Chungu 4
CR Belouizdad
Kaizer Chiefs
Teungeuth
MC Algiers