Simba Leo Kufa na Kupona...Manara Atangaza Vita Kubwa Kushinda ni Lazima

 


LEO Januari 6, Simba ina kibarua kigumu cha kusaka ushindi mbele ya Klabu ya FC Platinum kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambao ni wa marudio.

Rekodi zinaonyesha kwamba Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ndani ya dakika 180 kwenye mechi za kimataifa ambazo wamecheza Uwanja wa Mkapa mambo yamekuwa magumu kwao kupata ushindi.


 Safu ya ulinzi inayoongozwa na Pascal Wawa imeonekana kuwa bora kwa kuwa imeweza kufunga na kuruhusu bao moja ndani ya dakika 180 huku ile safu ya ushambuliaji inayoongozwa na John Bocco ikipambana dakika hizo bila kuambulia bao.


Mechi mbili za kimataifa Simba imekuwa na rekodi mbovu kwa safu ya ushambuliaji kuweza kufunga ndani ya dakika 90.


Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo, Agosti 28,2019 Simba ilikamilisha dakika 90 kwa sare ya kufungana bao 1-1, bao la Simba lilifungwa na kiraka Erasto Nyoni kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Miraj Athuman. 


Simba ilifungashiwa virago jumla kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali na Kocha Mkuu,  Patrick Aussems raia wa Ubelgiji baada ya kuiongoza timu kwenye mechi 10 za Ligi Kuu Bara alichimbishwa.


Pia hivi karibuni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo wa marudio dhidi ya Plateau United,Uwanja wa Mkapa, Desemba 5,2020 dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufungana.


Leo Simba ina kazi ya kufanya Uwanja wa Mkapa kuvunja rekodi hiyo kwa kuandika rekodi mpya ya kupata ushindi na ikiwa itapoteza kwa kufungwa itakuwa ni mara ya kwanza kupoteza kwa Mkapa kwenye mechi za kimataifa.


Sven amesema kuwa wanatambua kazi itakuwa ngumu ila watapambana kusaka matokeo ndani ya uwanja ili waweze kusonga mbele.


Mchezo wa kwanza Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe hivyo leo inatakiwa kushinda mabao zaidi ya mawili ili kutinga hatua ya makundi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad