Simba yafanya balaa kwa Mkapa, yamtandika FC Platinum 4-0




KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Januari 6 kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 
Simba imepata matokeo hayo ikiwa nyumbani na kufanikiwa kupindua meza kibabe baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kufungwa bao 1-0.

Bao la kwanza, Uwanja wa Mkapa lilifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 39 kwa mkwaju wa penalti baada ya Shomari Kapombe kuchezewa faulo ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti. 

Licha ya wachezaji wa FC Platinum kuonekana wakilalamika mwamuzi aliamuru ipigwe penalti na bao la pili lilifungwa na Shomari Kapombe dakika ya 62.

Bao la tatu ilikuwa ni John Bocco dk 90+1 na msumari wa nne ni Clatous Chama kwa penalti dakika ya 90+5 na kuifanya Simba itinge hatua ya makundi.

Wakiwa ugenini walifungwa na Perfect Chikwende ambaye leo aliwekwa kwenye uangalizi wa Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ambao walikuwa wakibadilisha kuweka ulinzi ndani ya Simba.

Sera ya WIDA,(War In Dar) imekubali baada ya Simba kupndua meza kwa kuwa FC Platinum ya Norman Mapeza ilipania kumaliza mchezo huu Uwanja wa Mkapa ila mambo yalikuwa magumu kwao.


Kazi ya kwanza imekamilika sasa ni kazi kwenye hatua ya makundi ambayo ina ushindani mkubwa kutoka timu kubwa ambazo zimewekeza mkwanja mrefu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad