Hatua ya nusu Fainali ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi zitachezwa
leo Jumatatu katika Uwanja wa Amaan kati ya Azam FC vs Yanga Sc
Saa 10:15 jioni na Simba Sc vs Namungo FC saa 2:15 Usiku .
Hayo ni Mashindano ya 15 tangu yalipoanzishwa rasmi mwaka 2007 ambapo
Simba Sc na Mtibwa Sugar zinaongoza kucheza fainali nyingi zikicheza
mara 6 kila timu.
Simba ambayo imecheza fainali 6, tatu ikitwaa Ubingwa na 3 ikipoteza
(2008,2011,2015,2017,2019 na 2020).
Mtibwa Sugar nayo imecheza fainali nyingi (6) za Mashindano hayo ambapo
wameshinda 2 na kupoteza 4 (2007, 2008, 2010, 2015, 2016 na 2020).
Azam ikishika nafasi ya tatu kucheza fainali nyingi za Mashindano hayo
ambapo imecheza fainali 5 na zote imetwaa Ubingwa (2012, 2013, 2017, 2018 na 2019.
Yanga wamecheza fainali 2 wakishinda 1 na kupoteza 1 (2007 na 2011)
sawa sawa na URA ya Uganda ikicheza fainali 2 wakishinda 1 na wakipoteza 1 (2016 na 2018).