Suma Lee Afunguka Kifo cha CPWAA





ALIYEKUWA msanii wa muziki wa Kizazi Kipya kisha kumrejea muumba wake kwa kujikita kwenye imani ya Dini ya Kiislam, Ismaili Saidi a.k.a Suma Lee ameelezea mateso aliyopitia rafiki na mwanamuziki mwenzake, Ilunga Khalifa almaarufu Cpwaa ambaye waliwahi kuwa kundi moja.

 

Suma Lee na Cpwaa ndiyo waanzilishi wa Kundi la Park Lane ambalo lilitisha na nyimbo mbalimbali tangu mwaka 2007.


Ilunga Khalifa almaarufu Cpwaa enzi wa uhai wake.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA baada ya kifo cha Cpwaa, Suma Lee anasema kuwa, mara kadhaa wakiwa kwenye shoo hata mikoani, kuna kipindi jamaa huyo alikuwa akibanwa na mbavu na kushindwa kupumua, jambo lililosababisha wakati mwingine ashindwe kupanda jukwaani.

 

“Jamaa kwa kweli huu ugonjwa uliomuua haukuwa mgeni kwake, ulikuwa ukimsumbua mara kwa mara na kuna kipindi nakumbuka siku moja tukiwa mikoani alizidiwa na kushindwa kupanda jukwaani ingawa mwisho wa yote mashabiki waliweza kutuelewa kwa kuwa wao wenyewe walimuona eneo la tukio.

 

“Hivyo kinachotakiwa kiimani tumuombee mwenzetu maisha mema ya pepote astarehe kwenye makazi yake ya milele,” anasema Suma Lee ambaye kwa sasa amesema anapenda aitwe Shehe Ismaili na kulikana lililokuwa jina lake la kimuziki la Suma Lee.

 

Cpwaa alifariki dunia hivi karibuni na kuzikwa katika Makaburi ya Mwinyimkuu yaliyopo Magomeni jijini Dar, jirani na nyumbani alipokuwa akiishi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad