ALIYEWAHI kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amefunguka kuwa hana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote kutoka Simba wakiwemo Clatous Chama na Luis Miquissone kwenda katika timu yake mpya ambayo amejiunga nayo.
Sven hivi karibuni alijiunga na timu ya Far Rabat ya nchini Morocco mara baada ya kuondoka ndani ya Simba ikiwa ametoka kuipeleka timu hiyo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na Championi Jumamosi,kocha Sven alisema kuwa, hana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote wa Simba kwani kuna wachezaji wengi wazuri ambao anawajua wa kuwasajili ndani ya timu hiyo tofauti na wale ambao wapo Simba.
“Nimefundisha Afrika kwa muda kidogo, nawafahamu wachezaji wengi wazuri ambao nina uhakika wakisajiliwa hapa Far Rabat watafanya vizuri tofauti na wale ambao wanapatikana Simba, watu wanaongea kuwa nitawasajili wachezaji wa Simba lakini si ukweli kuhusu hilo.“
Kwa sasa mipango ni kuangalia nini nitafanya nikiwa na timu yangu mpya ili kuifanya ifanikiwe katika Ligi Kuu ya Morocco na wala sifikirii tena nyuma kwa kuwafuatilia wachezaji wa Simba,” alisema kocha huyo.
Stori: Marco Mzumbe,Dar es Salaam