Tajiri wa Samsung afungwa miaka miwili na nusu jela




Bilionea wa kampuni kubwa ya vifaa vya kielektroniki nchini Korea Kusini Lee Jae-yong amerejeshwa gerezani hii leo baada ya mahakama nchini humo kumhukumu kifungo cha miaka miwili na nusu kutokana na kuhusika kwake kwenye kashfa ya uifsadi ya mwaka 2016 iliyosababisha maandamano na kuondolewa rais wa wakati huo Park Guen-hye. 
Mahakama ya juu ya Seoul imemkuta na hatia ya kumpa rushwa rais Guen-hye pamoja na mwandani wake ili kupata uungwaji mkono wa serikali kwenye makubaliano makubwa ya kibiashara baina ya washirika wa Samsung. 

Makubaliano hayo yangemsaidia Lee kuimarisha udhibiti wake kwenye kundi hilo kubwa kabisa la kibiashara nchini Korea Kusini. 

Mawakili wa Lee wamemuelezea mteja wao kama muhanga wa matumizi mabaya ya mamlaka ya rais na kuongeza kuwa makubaliano hayo yalikuwa ni ya kawaida ya kibiashara

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad