Magari yanayotoka nje ya nchi yatashushwa kwa utaratibu maalumu kutoka kwenye meli na kwenda kuwekwa kwenye eneo lake la maegesho ambalo limepangwa ndani ya bandari kwaajili ya ukaguzi.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania, Bw.Lazaro Msasalaga akitoa ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa magari yanayotoka nje ya ya nchi.
Akizungumza na wanahabari Bw.Msasalaga amesema bandarini kuna sehemu nne za kuegesha magari yanayoshushwa kwenye meli ambayo ni rore yard ni eneo ambalo linachukua magari madogo madogo na ndio eneo ambalo meli za magari zinaahusha.yard hii ikijaa magari madogo kuhamishwa kwenyw yard ya pili inayoitwa kitopeni pia kuna yard mbili ambazo zinahusika namagari makubwa yard ya kwanza inaitwa copper na nyingine inaitwa Lighter key.
“Kwa utaratibu wa namna magari yatakuwa yanashushwa na kuwekwa kwenye maeneo yake maalumu kutakuwa na seti za vifaa vya ukaguzi 12, lakini kwenye hizo seti 8 zitafungwa ndani ya rore yard . Seti mbili zitafungwa kwenye yard ya magari makubwa wakati seti moja itafungwa Kitopeni kwenye magari machache ambayo yamehamishwa kutoka rore yard”. Amesema Bw.Msasalaga.
Pamoja na hayo Bw.Msasalaga amesema wamehakikisha ndani ya bandari maeneo yote ambayo yanaegesha magari ambayo yanaingia kutoka nje ya nchi yatapata huduma ya ukaguzi bila kujali gari kubwa au dogo.