Tozo ya Tsh Milioni 1 kwa Magari ya Misiba Yapingwa Arusha




TOZO mpya ya shilingi milioni moja kwa magari yanayokodishwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo ya kubeba miili ya marehemu inayosimamiwa na (LATRA) imepingwa na wadau wa usafirishaji jijini Arusha ambao wameiomba serikali kuangalia upya suala hilo.

 

 

Mjadala huo umeibuka kwenye kikao cha watendaji wa LATRA na wadau hao ambao wamewalalamikia watendaji wa idara zinazosimamia biashara hiyo ikiwemo LATRA kuwa zinaendelea kuwakandamiza badala ya kuwasaidia.

 

 

Meneja leseni kutoka Mamlaka Ya Udhibiti Usafiri Wa Ardhini (LATRA), Bw.Leo Ngowi na mkurugenzi wa huduma za usafiri wa wizara ya ujenzi na uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka wamewataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu na kuendeea kutoa ushirikiano na mapendekezo kwani yote yatazingatiwa.

 

 

Kwa sasa huduma za magari ya kukodisha yakiwemo yanayobeba watu wanaokwenda kwenye harusi ama kwa shughuli za misiba na pia yanayobeba miili ya watu wanaofariki asilimia kubwa zinatolewa na magari ya kawaida yakiwemo yanayotumka kubeba abiria na mizigo utaratibu ambao sheria hiyo ikipitishwa hautakuwepo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad