Rais anayeondoka madaraka Donald Trump amsamehe aliyekuwa mshauri wake Steve Bannon, ambaye anakabiliwa na mashitaka ya udanganyifu.
Tangazo hilo linawadia saa kadhaa kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden.
Bwana Trump pia amewahurumia watu wengine zaidi ya 140 saa zake za mwisho madarakani.
Miongoni mwa waliosamehewa ni rapa Lil Wayne huku rapa mwingine Kodak Black na aliyekuwa meya wa Detroit Kwame Kilpatrick wakipunguziwa vifungo vyao.
MARE
Kwa ujumla watu 73 wamepewa msahamaha huku wengine 70 vifungo vyao vikapunguzwa, taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imesema. Bwana Bannon, ambaye alikuwa mshauri mkuu wa Rais Trump wakati wa kampeni yake mwaka 2016, alipatikana na hatia mwaka jana kwa makosa ya udanganyifu juu ya kampeni ya kuchangisha pesa kujenga ukuta katika mpaka ya Marekani na Mexico.
Waendesha mashitaka Bwana Bannon na wengine watatu walilaghai wengine mamia ya maelfu ya wafadhili kuhusiana na mradi wa “Tujenge Ukuta” kampeni ambayo ilikusanya dola milioni 25.
Inadaiwa kuwa Bwana Bannon alipokea zaidi ya dola milioni 1 ambazo baadhi ya pesa hizo alizitumia kwa matumizi yake binafsi.
Alikanusha makosa hayo na alikuwa ahukumiwe. Ikulu ya Marekani imesema Bwana Bannon amekuwa “kiongozi muhimu na anajulikana kwa hekima yake katika siasa”.
Taarifa hiyo ilisema kwamba waendesha mashitaka walikuwa wamemfungulia mashitaka yenye kuhusishwa na ulaghai kutokana na kujihusisha kwake kwenye mradi wa siasa.