Uchaguzi Uganda Hapatoshi Leo, Mvutano wa Kizazi Cha Jana na Leo

 


Raia wa Uganda leo wanashiriki katika zoezi la  kihistoria la upigaji kura ili kuchagua rais na wabunge wa kuliongoza taifa hilo.



Kulia Mgombea wa urais wa Uganda Yoweri Mseveni (NRM), na kushoto ni mgombea wa urais wa uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu


Katika maeneo mbalimbali ya Uganda milolongo mirefu imeshuhudiwa katika vituo vya kupigia kura ikiashiria kuendelea kwa zoezi la upigaji kura ambalo linatarajia kukamilka saa kumi jioni kwa saa za Uganda, ingawa Tume ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa wapigakura wote waliojisajiri ambao watakuwa bado katika mstari wa kupiga kura wataruhusiwa kupiga kura yao


Wanaowania nafasi ya urais ni wagombea 11 akiwemo mwanamke mmoja huku upinzani mkali ukionekana dhidi ya wagombea wawili ambao ni Yoweri Museveni wa chama cha National Resistance Movement (NRM), anayetetea kuongoza Uganda kwa muhula mwingine wa sita na  mwanamuziki, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine.


Aidha baadhi ya wadau wa masuala ya siasa na viongozi wamekuwa na mitazamo mbalimbali kuhusiana na uchaguzi ambapo wamesema kwenye uchaguzi huu kuna vizazi viwili vina vutana ambavyo ni kizazi cha jana na kizazi cha leo ambacho kinaona matatizo yaliyopo yamesababishwa na kizazi kilichopita.


Uganda ipo kwenye uchaguzi huku waangalizi wa uchaguzi wa marekani wakiwa wamezuiwa kuingia nchini sambamba na mitandao ya kijamii ikiwa imefunguwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad