Uganda: Msafara wa Mgombea Urais Washambuliwa kwa Risasi




Polisi mmoja nchini Uganda anazuiliwa katika kituo cha polisi kwa sababu ya kuupiga risasi msafara wa mgombea wa urais, Patrick Amuriat, Jumatano magharibi mwa eneo la Kitagwenda.

 

Polisi imesema afisa aliyekamatwa hakuwa amepewa jukumu la kumfuata Bwana Amuriat katika msafara wake wa kampeni, kulingana na taarifa ya gazeti la Daily Monitor.

 

Kituo cha televisheni cha eneo NTV, kimeandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter unaoonesha kilichofuata baada ya tukio hilo.

 

Raia wa Uganda Alhamisi ijayo watapiga kura kuchagua wabunge na rais huku Rais Yoweri Museveni akitafuta kuchaguliwa tena kwa muhula wa sita.

 

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameshutumu vikosi vya usalama kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano na mikutano ya kisiasa. Mwezi uliopia, mlinzi wa mgombea mwingine wa kisiasa Bobi Wine, alifariki dunia baada ya kukanyagwa na gari la jeshi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Similar Mafundisho ya Lobaati kwa Lobati kama alivyo fndishwa msaliti tundu.

    Tumepigwa mabomu kkweli kweli..!!? Bomu ukipigwa huwa halikosei.

    Tafuta kolabo na Dulla Makabila kama Hamolapa kakutolea nje.

    Mwache Kidume M7 aendeshe nchi. Amesha leta Airbuss we hata
    KIBAJAJI KWAKO ITAKUWA MTAJI WA PLODAKSHENI STUDIO.

    Uganda Oyeeee.
    Yoweri Kaguta Museveni Oyeeee.

    Lobati Ansata Damu ..Mhhh
    Lobati Kiagulanyika...Mhh..Mhhhh.

    Pipo...Pwaaahh...pwa pwa pwaaaa..!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad