Uganda yaishutumu Facebook kwa kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo




Afisa wa serikali nchini Uganda, ameishutumu kampuni ya Facebook akidai inaingilia masuala ya uchaguzi wa rais katika taifa hilo la Afrika Mashariki.Shutuma za afisa huyo zimejiri baada ya Facebook kufunga akaunti kadhaa zinazohusishwa na kampeni za Rais Yoweri Museveni kwa madai ya matendo yasiyo rasmi.
Msemaji wa rais Don Wanyama ameliambia shirika la Habari la Associated Press kwamba hatua ya Facebook ni Ushahidi wa kile maafisa nchini Uganda wanatizama kama uungwaji mkono kutoka nje unaoelekezwa kwa Bobi Wine ambaye ni mshindani mkuu wa Museveni kuelekea uchaguzi wa rais ambao umepangwa kufanyika Alhamisi wiki hii.Facebook imesema imefunga akaunti na kurasa kadhaa zilizokuwa bandia na kwamba zilitumiwa kwa lengo la kushawishi upigaji kura.

Akaunti zilizofungwa ziliendeleza kampeni kali dhidi ya mshindani wa Museveni Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine mwenye umri wa miaka 38

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad