Uganda yaishutumu Marekani 'kuingilia uchaguzi wake '




Msemaji wa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo, ameishutumu Marekani kwa kujaribu "kupindua matokeo ya uchaguzi", kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters.
Balozi wa Marekani nchini Uganda Natalie Brown Jumatatu alizuiwa kumtembelea kiongozi wa upinzani, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, nyumbani kwake mjini Kampala.

"Kile ambacho amejaribu kufanya wazi kabisa, ni kuingilia siasa za ndani za Uganda, hasa uchaguzi, kubadilisha matokeo ya uchaguzi na mapenzi ya watu," Bwana Opondo amezungumza na shirika la Reuters.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jumatatu ilitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi "wenye kujitegemea, wa uhakika, usiopendelea upande wowote, na wa kina" juu ya taarifa nyingi za uhakika" kuhusu wizi wa kura katika uchaguzi wa Uganda uliofanyika wiki iliyopita.

Rais Yoweri Museveni, aliyeshinda uchaguzi kwa awamu ya sita, amekanusha madai ya wizi wa kura.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Male kani wana yao ya kima lekani YANAWASHINDA.

    Unganda tuna yetu ya Kiganda.. Tunayamudu.

    TUSIBBABAISHANE. MALIZENU YENU KWA FAIDA YENU.
    YETU TUWACHIENI WENYEWE UMESIKIA BIBI BROWN. WAPE SALAM.
    Biden anaingoja nchi, Mpeni kwa Salama na Amani.

    Uganda Oyeeee.
    Museveni Oyeee.
    EAC Oyeeee.

    AFRIKA OYEEEEE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad