DAR: Sexy lady kunako Bongo Flevani, Mariane Mdee almaarufu Mimi Mars, kwa mara nyingine amejitokeza na kutupilia mbali tetesi na uvumi ambao umekuwa ukienea kuwa dada yake, Vanessa Mdee ‘V-Money’ kwa sasa ana mimba ya mchumba’ke, Rotimi.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Mimi Mars ameanika ukweli kwamba, Vanessa au Vee hana mimba kama watu wengi wanavyoeneza kwenye kurasa za udaku za Instagram kwa kumuangalia tu Vanessa kwenye picha.
Kwa mujibu wa Mimi Mars, Vee angekuwa na ujauzito angekuwa ameshamwambia kwani ni mtu ambaye anazungumza naye mambo mengi kuanzia kikazi, kifamilia na hata mambo yao ya siri wanashirikishana.
“Ukweli ninao mimi, Vee hana mimba, angekuwa nayo angeshaniambia,” anasema Mimi Mars.
Mimi anasema kuwa, wakati wa Vee kupata ujauzito ukifika atafanya hivyo.
Hii ni mara ya pili kwa Vanessa kusemekana kuwa ni mjamzito.
Mwaka jana alipodaiwa kuwa mjamzito alijitokeza kwenye kurasa zake za kijamii na kuandika;
“No sina mimba bado…”