Wachezaji 29 wa timu ya Taifa Stars wanaocheza ligi za ndani barani Afrika (CHAN) wapimwa vipimo vya moyo




Mtaalamu wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay akimpima kipimo cha damu mchezaji wa timu ya  Taifa Stars anayeshiriki mashidano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani Afrika (CHAN) Ibrahim Ame Mohamed . Wachezaji 29 wa timu hiyo  walifanyiwa  vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi  na damu ikiwa ni mojawapo ya kutelekeza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashidano hayo kupima.



Na Ntiba Nongwe -  Dar es Salaam

Wachezaji 29 wa timu ya Taifa Stars wanaocheza ligi za ndani barani Afrika (CHAN) wamepima vipimo vya moyo  ikiwa ni mojawapo ya kutelekeza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashidano hayo apime vipimo hivyo.

Upimaji wa vipimo hivyo umefanyika hivi  karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo wachezaji hao walipimwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography) umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiograph) na vipimo vya damu.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa kurugenzi ya tiba shirikishi Dkt. Delila Kimambo alisema ni jambo jema kwa wachezaji hao kupima vipimo vya moyo, kwa kufanya hivyo kutawasaidia kujua kama wanatatizo au la na kama wanamatatizo wataweza kuanza tiba mapema na kama hawana watafuata ushauri wa wataalamu wa afya wa jinsi ya kutunza mioyo yao.

Dkt. Delila ambaye pia ni daktari bingwa wa magojwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete alisema mara kwa mara wanawapima wachezaji kutoka vilabu mbalimbali vya mpira ambao wanashiriki mashidano ya kimataifa jambo linalowafanya wachezaji hao kucheza mpira bila hofu kwani wanajijua afya zao zikoje.

“Ninawasihi wachezaji wanaoshiriki michezo mbalimbali kupima afya zao kabla hawajaendelea na mashindano pia kwa upande wa timu zinazoshiriki ligi mbalimbali hapa nchini zije kupima kwa kufanya hivyo wachezaji wao  wataweza kushiriki mashindano vizuri “, alisisitiza Dkt. Delila.

Kwa upande wake meneja wa Taifa Stars Nadir Haroub maarufu kama  Canavaro alisema upimaji wa wachezaji hao ni maelekezo kutoka CAF hivyo basi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linasimamia upimaji huo ili wachezaji wapimwe na kutambuliwa afya zao.

“CAF  wanasisitiza wachezaji wapimwe afya zao ili wawe na uhakika nao wakiwa na wasisiwasi na majibu ya vipimo vya mchezaji wanarudia vipimo hivyo. Ndiyo maana kama mnavyowaona wachezaji wetu wamekuja kupima katika taasisi hii”, alisema Haroub.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ni Hospitali iliyothibitishwa na CAF  kuwa inakidhi vigezo vyote vya upimaji wa magonjwa ya moyo. Uthibitisho huo ulitolewa kabla ya kuanza kwa mashindano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yaliyofanyika mapema mwaka jana hapa nchini . JKCI ilikaguliwa na kuthibitishwa na wakaguzi kutoka CAF.

Timu mbalimbali zimeshafanyiwa vipimo hivyo katika Taasisi hiyo zikiwemo Taifa Stars wakati inashiriki mashidano ya mataifa ya Afrika , Timu ya Simba na timu ya Taifa ya soka la ufukweni.



Mchezaji wa timu ya  Taifa Stars anayeshiriki mashindano ya wachezaji  wanaocheza ligi za ndani barani Afrika (CHAN) Shomari Kapombe akimsikiliza mtaalamu wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay kabla hajampima kipimo cha damu. Wachezaji 29 wa timu hiyo  walifanyiwa  vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi  na damu ikiwa ni mojawapo ya kutelekeza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashidano hayo kupima vipimo hivyo.


Mchezaji wa timu ya  Taifa Stars anayeshiriki mashidano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani Afrika (CHAN) Juma Kaseja akisubiri kufanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi  na damu na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) . Wachezaji 29 wa timu hiyo wamepima vipimo hivyo  ikiwa ni mojawapo ya kutelekeza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashidano hayo kupima.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad