Idadi inayoongezeka ya wajumbe wa Republican wanaungana na juhudi za Rais Donald Trump za kuubatilisha uchaguzi, wakiapa kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo wakati Bunge litakapoandaa kikao wiki ijayo cha kuhesabu kura za wajumbe maalum maarufu kama Electoral College na kuidhinisha ushindi wa Rais mteule Joe Biden.
Seneta Ted Cruz wa jimbo la Texas ametangaza muungano wa maseneta 11 na maseneta wateule ambao wamedhamiria kuyapinga matokeo hayo katika kikao cha pamoja cha mabaraza yote mawili ya bunge Jumatano ijayo.
Kiongozi wa Warepublican katika Seneti Mitch McConell alikiomba chama chake kutojaribu kukibatilisha kile ambacho maafisa wasioegemea chama chochote wamesema ni uchaguzi uliokuwa wa huru na haki.