Wanafunzi 10 Bora Kitaifa Matokeo ya Kidato cha Nne 2020




Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne huku wavulana wakiongoza katika orodha ya wanafunzi 10 bora.

 

Katika orodha ya wanafunzi 10 bora, wavulana wapo saba na wasichana watatu. Matokeo hayo yametangazwa leo Ijumaa Januari 15, 2021 na katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.

 

Shule ya sekondari Cannosa ndiyo iliyong’ara zaidi kwa kuingiza wanafunzi watatu kwenye 10 bora. Kulingana na orodha hiyo, Paul Luziga wa Panda Hill ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na msichana Justina Gerald wa Canossa.

 

Mwanafunzi wa tatu ni Timothy Segu wa (Mzumbe), Isaya Rukamya(Feza Boys), Ashraf Ally (Ilboru), Samson Mwakabage (Jude), Derick Mushi (Ilboru).

 

Wengine walioingia kumi bora ni Layla Atokwete (Canossa), Innocent Joseph (Mzumbe) na nafasi ya 10 ikishikwa na Lunargrace Celestine wa Canossa.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad