Wanajeshi wavamia nyumbani kwa Bobi Wine


 


Mgombea wa urais nchini Uganda Bobi Wine, amesema kwamba wanajeshi wamevamia nyumbani kwake na kukamata walinzi wake, zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu. Msemaji wa polisi Kampala, Patrick Onyango, amekanusha madai hayo ya wanajeshi kuvamia nyumbani kwa Bobi Wine, akisema kwamba hakuna mtu aliyekamatwa, akielezea kwamba maafisa wa usalama wanaweka tu mikakati ya kiusalama katika sehemu zilizo karibu na nyumbani kwa Bobi Wine. Bobi Wine pia ameambia waandishi wa habari kwamba mmoja wa madereva wake alipigwa risasi na wanajeshi Jumatatu, na akafariki jumanee asubuhi wakati akipata matibabu. "Mmoja wetu ambaye wakati mwingine huwa dereva wetu na fundi wa magari yetu, ambaye ni Katerega, alipigwa risasi na wanajeshi na kufariki asubuhi hii. Nyumba yangu imevamiwa asubuhi hii na wasaidizi wangu wawili wamekamatwa. Mlinzi wangu amepigwa vibaya sana.” amesema Bobi Wine. Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu alhamisi wiki hii, zimesheheni msako mkali wa polisi na wanajeshi dhidi ya wagombea wa upinzani. Maafisa wanasema wanakamatwa wanaovunja maagizo ya tume ya uchaguzi, namna ya kudhibithi maambukizi ya virusi vya Corona. Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamesema kwamba maafisa wa serikali wanatumia janga la virusi vya Corona kuhangaisha wanasiasa wa upinzani. Japo matukio ya maafisa wa polisi na jeshi wamekuwa wakitumia nguvu dhidi ya wagombea wa upinzani katika chaguzi za miaka ya nyuma, matukio katika uchaguzi huu yamekuwa mabaya zaidi. Watu 54 waliuawa mnamo mwezi Novemba, wanajeshi na polisi walipokabiliana na wandamanaji baada ya Bobi Wine kukamatwa na polisi akiwa katika kampeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad