Mvutano ni mkubwa nchini Urusi baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Aleksey Navalny.
Maelfu ya wafuasi wa Navalny wameingia barabarani katika miji mingi.
Waandamanaji waliokusanyika katika uwanja wa Pushkin katika mji mkuu wa Moscow (Ikulu ya Rais) walitaka kutembea kwenda Kremlin. Walakini, polisi waliwazuia waandamanaji.
Waandamanaji wameandamana wakimkosoa Rais Vladimir Putin na kupiga kelele "Uhuru kwa Navalny".
Zaidi ya watu 360 wamekamatwa kote nchini.
Navalnıy, ambaye alipanda ndege kutoka Tomsk, Urusi kwenda Moscow mnamo Agosti 20 mwaka 2020 alibadilikiwa ghafla wakati yupo ndani ya ndege na kisha ndege ikalazimika kutua katika mji wa Omsk.Alikimbizwa hospitalini haraka na baadaye ikagundulika kuwa Navalny alichanganyiwa sumu kwenye chai yake.
Navalnıy alihamishwa kutoka Omsk kwa ndege ya kibinafsi kwenda Hospitali ya Charite huko Berlin, Ujerumani, mnamo Agosti 22.
Navalnıy alizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Moscow mnamo Januari 17 2021 mara tu aliporudi kutoka Ujerumani, alikokuwa akipokea matibabu.
Korti imeamuru Navalnıy kuzuiliwa kwa siku 30 hadi Februari 15, kwa madai kwamba "alikiuka kipindi cha probation mara kwa mara tangu Desemba 29, 2020".