Wananchi Wagoma Kufungiwa Mita za Maji

  


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kalela wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wametishia kutotumia maji yanayotolewa na mradi wa maji uliojengwa katika eneo hilo kama hatua ya kugomea kufungiwa mita kwa madai ya kuwa gharama za matumizi yake haziendani na kipato chao.

 

Hali hiyo ya azma ya kupinga matumizi ya mita imejitokeza wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye, wakati akikagua miradi ya maji.


Baadhi ya wanachi hao akiwemo Edson Mzana na Ernest Nyamurugwa, wamesema kwakuwa wao katika maeneo yao kuna mito mingi hivyo hawawezi kukubali kulipia maji ili hali kuna maji ya bure, huku wengine wakidai kuwa suala la kulipia huduma ya maji huwa wanalisikia likifanyika mjini pekee kwahiyo wao wanashangaa.


Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), wilaya ya Kasulu Mhandisi Edward Kisalu, amesema kuwa wananchi pia wamekuwa wakiharibu miundombinu ya mradi kama hatua ya kugomea kufungiwa mita.


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye, amesema utaratibu huo ni endelevu na umewekwa ili miradi ijiendeshe yenyewe na kuhudumia wananchi vizuri.


"Tunataka watu tuwaoneshe ustaarabu na kumiliki mradi kwamba ni wa kwao, na mita inachofanya ni kuhakikisha kila mtu anatumia maji kwa uangalifu"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad