Jeshi la Polisi Mkoani Arusha jana jioni lilitumia mabomu ya machozi ya kuwatawanya wanawake waliokuwa wakiandamana na kufunga barabara wakizuia kuzikwa kwa Anna Ng'ida aliyeuwawa kwa kunyongwa na kutupwa katika korongo .
Tukio hilo lilitokea jana jioni katika Kata ya Mateves nje ambayo ipo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Wakizungumza katika maandamano hayo,wanawake wao waliokuwa wanataka uchunguzi wa kina ufanyike juu ya kluhusiana na vifo vya wanawake tisa vilivyotokea hivi karibuni katika eneo hilo.
Wakizungumzia tukio hilo, Salina Haruni alisema wameshangazwa na kitendo cha kushambuliwa kwa mabomu wakati wao walikuwa wanataka uchunguzi wa vifo hivyo kufanyika.
"Huyuni mtu wa tisa kuuawa hatuoni jitihada za kukamatwa watuhumiwa," alilalamika Salina.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha , Salum Hamduni alieleza polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuweza kuwatawanya watu hao
Alisema kabla ya nguvu kutumika waliwataka watu hao kutawanyika lakini waligoma.
Hata hivyo, aliomba radhi kwa tukio hilo na kuahidi uchunguzi utafanyika kuwakamata watuhumiwa.
Baada ya majadiliano baina ya pande zote hatimaye mwili wa mwanamke aliyeuawa ulizikwa.