Watu wawili wamenusurika kifo nchini Kenya baada ya basi linalomilikiwa Pollman Tours na Safari Company kutumbukia katika bahari ya hindi katika feri ya likoni.
NATION
Mtandao wa Nation , umeandika kuwa basi liliteleza kutoka kwenye feri na kuingia ndani ya majira saa nne asubuhi ,hatua chache kabla ya eneo la nchi kavu.
Dereva na kondakta wameokolewa wote na polisi pamoja na walinzi wa kivuko.
Basi hilo la Yutong luxury lilikuwa linatokea Diani ambapo lilikuwa limewapeleka watalii waliowasili Mombasa hapo jana.
Ingawa kuna basi lingine kutoka kampuni hiyo hiyo lilifanikiwa kuingia kwenye feri likiwa salama.
Dereva wa basi hilo bwana Salim Omar amewaambia polisi kuwa alishindwa kulidhibiti gari kutumbukia majini baada kuanza kuteleza, na kulikuwa na mvua iliyonyesha majira ya asubuhi.
“Nilikuwa karibu nafika feri lakini basi likanizidi nguvu na kutumbukia, Ninamshukuru tu Mungu kuwa tuko salama,” alisema bwana Omar, ambaye alikuwa bad anatetemeka.
Alisema amekuwa akivuka likoni wakati anaendesha kwa miaka 11 na hajawahi kukutana na tukio la namna hii, hii ni mara ya kwanza.