Washtakiwa 57 wafutiwa mashtaka gereza la Kayanga

 


Jumla ya Washtakiwa 57 wanaume 54 na wanawake 3 wamefutiwa mashtaka katika Gereza la Kayanga, wakati Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju, pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Godfrey Mheluka walipotembelea na kukagua hali ya gereza hilo wilayani Karagwe Januari 21.


Biswalo amewaachia washtakiwa hao na kuwataka waliofutiwa mashtaka kujirekebisha na kwenda kuwa raia wema watakaporudi uraiani ikiwa ni pamoja na kujishulisha na shughuli za uzalishaji.




Washtakiwa wamefutiwa mashtaka mbalimbali yaliyokuwa yanawakabili ikiwepo wizi wa mifugo,ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi na ugomvi wa mipaka ya mashamba.


“Nendeni mkawe raia wema, badilikeni na msirudie tena kutenda uhalifu”. Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga.


Katika kundi la Washtakiwa walioachiwa huru wapo raia toka nchi jirani ya Burundi ambapo amewataka kufuata taratibu za kisheria endapo wanataka kuishi nchini.


Aidha Bw.Biswalo amewataka , Washtakiwa waliobaki gerezani kuendelea kujifunza na kubadilika wakati pia wakiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kuwasamehe na kuwafungulia nuru ili siku moja warejee uraia na kuendelea na maisha yao kama kawaida

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad