Watetezi wa haki za binadamu nchini Kenya wakamatwa nje ya ubalozi wa Uganda

Watetezi wa haki za binadamu wanne wa Kenya wamekamatwa nje ya ubalozi wa Uganda jijini Nairobi asubuhi muda mfupi kabla ya kuwasilisha taarifa yao kwa vyombo vya habari kuhusiana na ukatili wa polisi dhidi ya upinzani nchini Uganda.

Wanaharakati hao ambao kwa sasa wanashikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa na polisi ni pamoja na Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika, Hussein Khalid pamoja na mwandishi wa habari Yassah Musa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad