Watu 9 wafariki mwambao wa Msumbiji kufuatia kimbunga Eloise

 


Watu wasiopungua tisa wamefariki baada ya kimbunga cha kitropiki cha Eloise kupiga mwambao wa mashariki mwa Afrika wikendi hii. Kimbunga hicho kiliambatana na upepo wenye kasi ya kilomita 160 kila saa pamoja na mvua kubwa. 

 

Kulingana na maafisa wa serikali, vifo vingi vimeripotiwa katika mji wa bandari wa Beira nchini Msumbiji baada ya kuangukiwa na miti. Hata hivyo nguvu ya kimbunga hicho ilipungua wakati kikielekea nchi jirani za Zimbabwe, Botswana na baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini. 

 

Maafisa wamesema mtu mmoja aliuawa katika kisiwa cha Madagascar ambako kimbunga hicho kilianzia na kusababisha mafuriko. Kulingana na maafisa wa taasisi ya taifa ya Msumbiji kuhusu utabiri wa hali ya hewa (INAM) mji wa Beira ulipata mvua yenye kiwango cha milimita 250 ndani ya saa 24.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad