Wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule kuwekwa ndani





Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Onesmo Buswelu amesema atawaweka rumande wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto wao shule mpaka kufikia Januari 18, 2021.


Amesema hatakubali wala kuvumilia wazazi na walezi wa namna hiyo na kaahidi kutumia askari wa Jeshi la Akiba wilayani humo kuwakamata.



Akizungumza leo Ijumaa Januari 15, 2021 amesema wanafunzi wengi hawajaripoti shuleni na kuitaja shule ya Karansi kwamba wapo wanafunzi 163 ambao hawajaripoti.



Alieleza hayo wakati akikagua baadhi ya shule za wilaya hiyo pamoja na  kuangalia maendeleo ya wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza.



“Jumatatu tutaanza msako kuwakamata wazazi walioshindwa kuwapeleka watoto wao shule na nitawaweka ndani, hatuoni sababu ya mzazi kubaki na mtoto nyumbani wakati huu ambao anapaswa kuwepo shule.”



“Ikifika Jumatatu wale wote ambao watoto wao hawajaripoti  shuleni ni lazima tuwachukulie hatua kwa uzembe pamoja na kutotii maelekezo ya serikali, tunafanya hivyo kwa sababu rais (John Magufuli) ametoa fedha nyingi kuhakikisha watoto hawa wanasoma bila malipo. Majengo yapo, viti na meza vipo hatutaiona haya kuwakamata,”amesema Buswelu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad