Waziri Mkuu aongoza mazishi ya mtoto wa Nyerere

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki mazishi ya mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rosemary Nyerere aliyefariki dunia Januari Mosi, 2021.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwe udongo katika kaburi la Rosemary Nyerere ambaye ni Mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambara Nyerere katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika Kituo cha Hija Pugu Jijini Dar es Salaam, Januari 6, 2021.


Mazishi hayo ya Rosemary Nyerere yamefanyika leo Januari 6, 2021 katika makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo kwenye Kituo cha Hija kilichoko Pugu jijini Dar es Salaam.


Ibada ya mazishi imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Upanga jijini Dar es Salaam, Dias Mario. Viongozi wengine walioshiriki katika mazishi hayo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba.


Wengine ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula.


Viongozi wengine ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi, Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakary Kunenge na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad