Waziri Mkuu na Waziri wa Afya wajiuzulu kisa corona




Waziri Mkuu wa Mongolia Khurelsukh Ukhnaa amewasilisha barua ya kujiuzulu mbele ya Bunge leo kufuatia maandamano ya umma kulaani jinsi Serikali yake inavyoshughulikia janga la virusi vya Corona.
Shirika la Habari la Taifa limeripoti kuwa Ukhnaa amesema anachukua uamuzi huo kama sehemu ya kuwajibika na kuitikia matakwa ya umma yaliyochochewa na kile kinachotajwa kuwa unyanyasaji kwa wagonjwa wa COVID-19.

Maandamano makubwa yalizuka jana Jumatano baada ya kuvuja kwa mkanda wa video ulioonesha mwanamke mmoja na mtoto wake mchanga wakihamishwa kwa nguvu kwenda kituo cha karantini kinachoendeshwa na idara ya afya ya taifa.

Maandamano hayo yamechochea pia kujiuzulu kwa viongozi wengine wa serikali ikiwemo waziri wa afya na naibu waziri mkuu kwenye taifa hilo lenye zaidi ya visa 1,500 vya COVID-19.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad