Wenyeviti Kamati 14 za Bunge Kujulikana Leo Dodoma





UCHAGUZI wa Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge 14 utafanyika leo, baada ya vikao vya kamati hizo kuanza, jijini hapa.

 

Huu ni mchuano mwingine bungeni kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wa upinzani ambao wanatarajiwa kupambana kuwania kuongoza kamati za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambazo kwa mujibu wa kanuni za Bunge lazima ziongozwe na wabunge wa upinzani.

 

Ratiba ya kuanza vikao hivyo iliyotolewa na Ofisi ya Bunge jana, ilionyesha kuwapo kwa uchaguzi wa viongozi hao wa kamati 14. Kamati zingine ambazo zitafanya uchaguzi huo mbali na PAC na LAAC, ni pamoja na Viwanda, Biashara na Mazingira, Katiba na Sheria, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

 

Nyingine ni ya Utawala na Serikali za Mitaa, Huduma na Maendeleo ya jamii, Ardhi, Maliasili na Utalii, Kilimo, Mifugo na Maji, Miundombinu, Nishati na Madini, Sheria ndogo, Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) na kamati ya Bajeti.

 

Wiki iliyopita taarifa iliyotolewa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, ilisema kamati hizo zitakutana kutekeleza majukumu ya kibunge kuanzia leo hadi Januari 31, mwaka huu, kabla ya kuanza mkutano wa pili wa Bunge Februari 2, mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad