WHO: Wanasayansi waharakishe chanjo




Kwa kuzingatia vifo vya zaidi ya watu milioni mbili vilivyorekodiwa ulimwenguni kote kutokana na virusi vya corona, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeihimiza jumuiya ya kimataifa kuharakisha utafiti na chanjo. 
Hayo yamezungumzwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa na Kamati ya dharura ya WHO. 

Aidha, shirika la WHO limewataka wanasayansi ulimwenguni kote kufanya kazi kwa karibu zaidi ili kusaidiana maarifa ya kisayansi juu ya namna ya kukabiliana na aina mpya ya virusi hivyo vya corona iliyogunduliwa hivi karibuni. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema idadi ya vifo imekuwa kubwa kutokana na kukosekana kwa juhudi za uratibu ulimwenguni. Guterres amesema sayansi imefanikiwa, lakini mshikamano umeshindikana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad