MSHAURI Mkuu wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha kuelekea mabadiliko amesema kuwa wanazidi kupambana ili kufikia malengo na wanatambua kwamba kazi ni kubwa kufikia malengo jambo linalofanya wawepo wabaya ambao wanawafuatilia.
Mbatha alikuwa ndani ya Simba ambapo alikuwa Mtendaji Mkuu kabla ya kubwaga manyanga na kuibukia ndani ya Yanga.
Tayari amefanikiwa kutwaa taji la Mapinduzi ambalo ni la kwanza kwake akiwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze. baada ya kushinda kwa penalti 4-3 dhidi ya mabosi zake wa zamani ambao ni Simba.
Mbatha amesema:"Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa sasa ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa kuwa mipango mikubwa na lazima yatimie.
"Hatulali ili kufikia yale ambayo tunayatarajia kwa kuwa wapinzani wetu pia hawalali hivi karibuni tutawafichua wabaya wetu ili mashabiki waweze kuwajua," .