FISTON Abdulrazak raia wa Burundi amemalizana na mabosi wa Klabu ya Yanga ili kuongeza makali Kwenye safu ya ushambuliaji.
Abdulazack ambaye ni mshambuliaji yeye ni mshambuliaji ambaye anacheza pia timu ya Taifa ya Burundi.
Nyota huyo aliletwa duniani Septemba 5, 1993 ana umri wa miaka 27 anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa ndani ya Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo ikielezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili.
Walianza na Saido Ntibanzokiza kisha ikafuata Dickson Job na sasa ni zamu ya Abdulrazak.
Nyota huyo pia amewahi kucheza ndani ya Klabu ya ENPPI ya Misri ambapo jezi yake namba anayoipenda ni 12.
Kwenye timu ya Taifa ya Burundi amecheza jumla ya mechi 49 tangu msimu wa 2009 na ametupia mabao 19.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa lengo kubwa la kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambulia ni kufunga mabao zaid.