Serikali imesema chanjo itahifadhiwa mahali salama katika jimbo la Gauteng na kisha kusambazwa kwenye majimbo mengine.
Chanjo hiyo itaanza kutolewa hivi karibuni.
Waziri wa Afya nchini humo, Zweli Mkhize alichapisha picha kwenye mtandao wa twitter kuwasili kwa bechi ya kwanza.
Nchi hiyo ilipokea chanjo ya AstraZeneca lakini ilisitisha kutolewa kwa chanjo hiyo baada ya kuwepo mashaka kuhusu ufanisi wake dhidi ya aina ya kirusi cha nchini humo.
Lakini wataalamu wa chanjo wa Shirika la Afya duniani wamesema hata nchi zenye aina ya virusi ambavyo kwanza vilibainika Afrika Kusini watumie chanjo ya AstraZeneca vaccine.
Kituo cha kupambana na kuzuia magonjwa Afrika(CDC) pia wamependekeza matumizi ya chanjo hiyo.