Atletico Madrid na Chelsea kukipiga nchini Romania

 


Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, limethibitisha kuwa, mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano hatua ya 16 bora ya michuano hiyo kati ya Atletico Madrid ya Hispania na Chelsea ya England utachezwa Februari 23, 2021 nchini Romania na si nchini Hispania.

 


Mabadiliko hayo yametokana na taratibu za kujikinga na Covid-19 nchini Hispania ambazo zinalazimisha watu watokao nchini England, Afrika ya Kusini na Brazili yakiwa miongoni mwa mataifa yaliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo, kukaa karantini kwa siki 10 kabla ya kuingia zaidi nchini humo.


Hivyo, mchezo wa Atletico Madrid dhidi ya Chelsea uliopangwa uchezwe kwenye dimba la nyumbani la klabu ya Atletico Madrid, Wanda Metropolitano nchini Hispania, sasa utachezwa kwenye dimba la The National Arena nchini Romania ambapo watu hupimwa na kuingia nchini humo wakikutwa hawana Covid-19.


Uwanja huo si mgeni kwa Atletico Madrid, kwani mwaka 2012 watukutu hao wa kocha Diego Simeone walitwaa taji la Uefa Europa ligi baada ya kuwafungwa wahispania wenzao, klabu ya Athletic Bilbao kwa mabao 3-0.


Kwa upande wa nchini Ujerumani, na wenyewe wameweka utaratibu wa wageni hususani kutoka nchini Uingereza kukaa karantini siku 10 kabla ya kusafiri zaidi maeneo ya ndani ya taifa lake ili kuzuia maambukizi mapya ya ugonjwa huo hatari.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Kutokana na utaratibu huo, pia michezo ya klabu bingwa Ulaya kati ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani dhidi ya Manchester City ya England na RB Leipzig ya Ujerumani itakayokipiga na Liverpool, kwasasa zote zitachezwa nchini Hungary.

 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad