KLABU ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kesho itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Klabu ya TP Mazembe.
Januari 30, Azam FC ilishinda mabao 3-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 10 jioni.
Mabao ya Azam FC mawili yalifungwa na nyota wao Prince Dube na moja lilifungwa na Mudathiri Yahaya huku lile la KMC likifungwa na Lusajo Mwaikenda.
Kesho Februari 2 Azam FC inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya miamba ya Afrika, TP Mazembe ambao ni washindi wa tatu wa mashindano ya Simba Super Cup.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo ya mchezo huo ni kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.
Azam FC ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo inatarajiwa kucheza Februari 7 na Simba ambao ni mabingwa wa Simba Super Cup, Uwanja wa Mkapa.
Ngoja wakutane na kichapo
ReplyDelete